1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Masoko ya hisa yahofia wimbi la pili la maambukizi ya Corona

Sekione Kitojo
11 Juni 2020

Mitaji imeporomoka katika masoko ya hisa kwa siku ya nne mfululizo baada ya hazina ya Marekani kutoa hali halisi ya uchumi  wa Marekani, hali inayoleta hofu kwa wafanyabiashara kote duniani.

https://p.dw.com/p/3dcw8
Bangladesch Ost Dhaka Lockdown Coronavirus
Picha: DW/M. Rashed

Wafanyabiashara  pia  wameguswa na  hofu ya  wimbi la  pili  la  maambukizi  ya  virusi  vya  corona nchini  Marekani  na  kwingineko duniani. Hii  ni  kutokana  na ongezeko  jipya  la maambukizi katika  baadhi  ya  majimbo.

Bangladesch Ost Dhaka Lockdown Coronavirus
Maafisa wameliweka eneo la mashariki mwa mji mkuu Dhaka, Rajabazar katika vizuwizi vya watu kusalia majumbani mwaoPicha: DW/M. Rashed

Masoko  ya  hisa  yamekuwa  yakifanya vizuri  kwa  wiki  kadhaa wakati  hatua  za  kuwazuwia  watu  kutoka  majumbani  mwao zikilegezwa  hatua  kwa  hatua  katika  maeneo muhimu,  na  baada ya  serikali  na  benki  kuu  za  nchi  kuahidi  matrilioni  ya  dola kusaidia  kuzindua  ukuaji  wa  uchumi  wao.

Lakini  baada  ya  mkutano  uliokuwa  ukitupiwa  jicho  kwa  karibu, wizara  ya  fedha iliweka mtazamo  wake  kwamba  uchumi  huo mkubwa duniani  utachukua  muda  kuweza  kurejea  kikamilifu  katika hali  yake  ya  kawaida  kutokana  na  dharura hii  ya  janga  la virusi vya  corona  ambalo  halijawahi  kushuhudiwa  kwa  vizazi  kadhaa, hali  ambayo  inatarajiwa  kuielekeza  dunia  katika  mdororo wa uchumi.

Jumla  ya  idadi ya  maambukizi ya  virusi  vya  corona  nchini Marekani imepindukia  milioni 2 hadi  jana, kwa  mujibu  wa  idadi iliyowekwa  pamoja  na  shirika  la  habari  la  Reuters, huku  shughuli za  kawaida zikirejea  hatua  kwa  hatua  katika  majimbo mengi.

Bildergalerie USA Los Angeles | Coronavirus | Ärztin Zafia Anklesaria
Mgonjwa wa COVID-19 nchini MarekaniPicha: Reuters/L. Nicholson

Maambukizi zaidi Urusi

Maambukizi  ya  virusi  vya  corona  nchini  Urusi  imepindukia  watu laki tano  leo  baada  ya  maafisa  wa  afya  kuripoti maambukizi mapya  yanayofikia  watu 8,779.  Urusi  ina  jumla  ya  wtu 502,436 waliothibitishwa  kuambukizwa  ugonjwa  wa  COVID-19, ikiwa  ni pamoja  na  vifo 6,532.

Licha  ya  kurekodi  karibu  maambukizi  mapya  9,000 kwa  siku kwa  zaidi  ya  mwezi  mmoja, maafisa  nchini  Urusi  wameanza kulegeza  vizuwizi vya  watu kusalia  majumbani  katika  majimbo mengi, ikiwa  ni  pamoja  na Moscow, ambayo  ina  asilimia  40  ya wagonjwa  wote  kwa  jumla na  karibu  nusu  ya  vifo  vilivyoripotiwa.

Serikali  ya  mji  wa  Tokyo  inapanga  kuruhusu  biashara kufunguliwa  tena kuanzia  Juni 19, wakiondoa  maombi  ya kuendelea  kuwazuwia  watu  kutoka  majumbani mwao iliyotoa  ili kudhibiti  kusambaa  kwa  virusi  vya  corona.

Chile Coronavirus in Santiago
Watu wakivalia barakoa kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona mjini Santiago, Chile.Picha: picture-alliance/Agencia Uno/F. Castillo

Tanzania yatakiwa kutoa data

India  imeripoti kiwango  cha  juu  cha  maambukizi  cha  karibu  watu 10,000  wapya  walioambukizwa  virusi  vya  corona leo, ambapo huduma  za  afya  katika  miji  iliyoathirika  zaidi  ya  Mumbai , New Delhi na  Chennai  ikiendelea  kupata  maambukizi  zaidi.

Mkuu wa  kituo cha udhibiti wa  magonjwa  barani  Afrika  amesema tunaendelea  kuwa  na  matumaini kuwa  Tanzania  itatoa  ushirikiano kwa  kutoa  data za  mambukizi  ya  virusi  vya  corona  nchini  humo hata  iwapo  rais  wa  nchi  hiyo John Pombe Magufuli  alitangaza ushindi  dhidi  ya  janga  hilo.

John Nkengasong  amesema  wanaelewa  maslahi  yaliyopo, katika taifa  hilo  la  Afrika  mashariki, ambalo  halijatoa  idadi  mpya  ya data  za virusi  vya corona tangu mwishoni  mwa mwezi Aprili.