1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashua ya wakimbizi wa kutoka Afrika imezama karibu na Sisilia nchini Italy

19 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDKI

Roma:

Mashua iliyokua na zaidi ya wakimbizi mia moja wa kiafrika imezama karibu na fukwe za Sizilia nchini Italy.Kwa mujibu wa askari wa ulinzi wa fukwe za Italy,watu wasiopungua sabaa wamekufa.Sehemu kubwa ya mabaki ya mashua hiyo imeokolewa.Mashua hiyo yenye urefu wa mita kumi,ilipinduka karibu na kisiwa cha Lampedusa.Kisiwa hicho cha kusini mwa Italy ni kivutio kikubwa cha wakimbizi wanaokusanyika Afrika kaskazini kwa lengo la kuingia Italy na baadae katika nchi nyengine za Ulaya.