1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Mashirika ya UN yasema Gaza yahitaji msaada zaidi wa dharura

15 Januari 2024

Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa wameonya Jumatatu kuwa Gaza inahitaji kwa dharura msaada zaidi au wakaazi wake wanaokabiliwa na hali ngumu watakumbwa na baa la njaa na magonjwa.

https://p.dw.com/p/4bGIr
Mashirika ya UN yasema uingizwaji msaada Gaza unaathiriwa kutokana na kufunguliwa kwa vivuko vichache vya mpakani.
Mashirika ya UN yasema uingizwaji msaada Gaza unaathiriwa kutokana na kufunguliwa kwa vivuko vichache vya mpakani.Picha: Mohammed Talatene/picture alliance/dpa

Wakati wakuu hao wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani - WFP, la kuwahudumia watoto UNICEF na la Afya Ulimwenguni - W.H.O hawakuitaja moja kwa moja Israel, wamesema uingizwaji msaada unaathiriwa kutokana na kufunguliwa kwa vivuko vichache vya mpakani, mchakato unaojikokota wa ukaguzi wa malori na bidhaa zinaoingizwa Gaza, na mapigano yanayoendelea kote katika ukanda huo.

Mashirika hayo yamesema njia mpya za kuingia Gaza zinapaswa kufunguliwa, malori zaidi yanapaswa kuruhusiwa kuingia kila siku, na wafanyakazi wa misaada na wale wanaotafuta msaada wanapaswa kuruhusiwa kusafiri kwa usalama.

Hayo yanajiri wakati maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na wanamgambo wa Hamas wakisema kuwa idadi ya vifo kutokana na vita kati ya Israel na Hamas imepindukia 24,000.