1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waangalizi: Hali Gaza imefikia kiwango cha kutisha

15 Februari 2024

Wakuu wa mashirika ya kiutu wamesema wameishiwa na maneno ya kuelezea maovu yanayoendelea huko Gaza, wakisisitiza kuwa mataifa na hasa Israel haiwezi kuwatwika wafanyakazi wa misaada mzigo wa umwagaji damu huo.

https://p.dw.com/p/4cRwy
Rafah, Ukanda wa Gaza | Mama akiwa na mwanae aliejeruhiwa
Mwanamke akiwa kampakata mwanae aliejeruhiwa na mashambulizi ya Israel katika eneo la Rafah, Ukanda wa GazaPicha: MOHAMMED ABED/AFP

Jumuiya ya kimataifa imeongeza shinikizo la kuupinga mpango wa Israel wa kufanya kile imekitaja "operesheni kubwa" kwenye mji wa Rafah ulio kusini mwa Gaza eneo ambalo zaidi ya Wapalestina milioni 1.5 wamekwama.

Mashirika ya kibinaadamu yanaonya kuwa kuendesha operesheni za misaada katika eneo hilo huenda isiwezekane kabisa hivi karibuni.

Soma pia:CPJ: Waandishi 99 waliuawa kufuatiamzozo wa Israel-Hamas

Wakuu wa shirika la msalaba mwekundu, Madaktari wasio na Mipaka, na lile la misaada la Umoja wa Mataifa wamewaambia mabalozi mjini Geneva kuwa hali huko Gaza inafikia kiwango ambacho haitzakuwa kosa la mashirika ya kiutu kama watu watateseka, bali itakuwa ni kosa la wale watakaoamua kuruhusu hilo kutokea.

Wakati hayo yakijiri, jeshi la Israel limesemalimewakamata wanamgambo kadhaa wa Hamas, lilipoivamia hospitali kuu ya mji wa kusini mwa Gaza wa Khan Younis. Operesheni hiyo kwenye hospitali ya Nasser ilisababisha kifo cha mtu mmoja.