1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashirika ya kiutu yadai Wakongo hawajafikiwa na misaada

12 Julai 2024

Wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kiutu na makundi ya kiraia wanasema mamilioni ya watu mashariki mwa Kongo bado hawajafikiwa na misaada licha ya mapigano kusitishwa kwa wiki mbili.

https://p.dw.com/p/4iDga
Baadhi ya wakimbizi waliokimbia vita kati ya M23 na jeshi la Kongo huko Sake, Magharibi mwa Goma.
Baadhi ya wakimbizi waliokimbia vita kati ya M23 na jeshi la Kongo huko Sake, Magharibi mwa Goma.Picha: Moses Sawasawa/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Wafanyakazi wa mashirika ya misaada ya kiutu na makundi ya kiraia wanasema mamilioni ya watu mashariki mwa Kongo bado hawajafikiwa na misaada licha ya mapigano kusitishwa kwa wiki mbili.

Wafanyakazi hao wanasema kipindi hicho cha wiki mbili ambacho wiki moja tayari imeshakwisha kamilika, hakitoshi.

Soma pia: AU walaani mauaji ya watu wengi nchini DR Congo

Mkuu wa afisi ya shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi, UNHCR, Abdoulaye Barry, anadai kwamba licha ya amri hiyo ya usitishwaji mapigano, kumekuwa na ripoti za machafuko katika eneo la Masisi karibu na mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma.

Wiki moja iliyopita, Marekani ndiyo iliyotangaza usitishwaji huo wa mapigano kwa wiki mbili na kuwapelekea waasi wa M23 wanaopambana na jeshi la kongo kuweka chini silaha zao.