1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Mashambulizi ya makombora ya Urusi yawaua watu 3 Ukraine

30 Januari 2023

Mashambulizi ya makombora ya Urusi yamewaua watu 3 kusini mwa Ukraine jana Jumapili katika wakati mapigano makali yanaendelea kwenye mkoa wa Donetsk ambako Urusi imeushambulia kwa mara nyingine mji muhimu wa Vuhledar.

https://p.dw.com/p/4MrXL
Russischer Angriff auf Cherson, Ukraine
Picha: GENYA SAVILOV/AFP/Getty Images

Maafisa wa Ukraine wamesema mbali ya watu 3 waliouwawa, wengine 6 wamejeruhiwa katika hujuma hizozilizoulenga mji wa Kherson na ambazo zimesababisha pia uharibifu wa jengo la shule na hospital kwenye eneo hilo.

Soma pia:Zelensky: 2023 utakuwa mwaka wa ushindi kwa Ukraine

Kupitia hotuba ya kila siku kwa taifa rais  Volodymyr Zelenskiy amesema Ukraine inapitia kipindi kigumu huko Donetsk na inahitaji msaada wa haraka wa silaha na aina mpya ya zana za kivita.

Amesema miji ya Bakhmut, Vuhledar na maeneo mingine ya mkoa wa Donetsk yanashuhudia mashambulizi makali ya Urusi anayoituhumu kuwa na malengo la "kuwafadhaisha na kuwavunja nguvu wapiganaji wa Ukraine"