1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa watu 5 kote Gaza

16 Julai 2024

Watu wasiopungua 50 wameuawa hivi leo katika ukanda wa Gaza kufuatia makabiliano makali kati ya vikosi vya Israel na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4iNbm
Gaza Chan Yunis 2024 |Mashambulizi ya Israel
Wapalestina wkasanyika katika eneo la shambulizi la Israel la Al-MawasiPicha: Hatem Khaled/REUTERS

Wizara ya afya ya Gaza imesema hadi sasa idadi ya vifo imefikia watu 38,713. Ahar Abu Emeira ni mkaazi wa Gaza. " Oh ulimwengu, tuokoeni! Si haki kwamba nyote mnatutazama hivi. Hii si haki kushuhudia idadi ya mashahidi wanaokufa kila dakika. Nyumba zinaharibiwa juu ya vichwa vya watu bila sababu yoyote. Mwenyezi Mungu ndiye anayenitosheleza, naye ndiye mlinzi aliye bora zaidi. Maneno hayatoshi kuelezea hili."

Soma zaidi: Israel yaendeleza mashambulizi ya anga na ardhini Gaza

Marekani ambayo ni mshirika na mfadhili wa Israel imekosoa ongezeko la vifo vya raia ambapo Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Antony Blinken amesisitiza kwamba vitendo hivyo havikubaliki.

Kundi la Hamas linaishutumu Israel kuzidisha mashambulizi yake ili kujaribu kukwamisha juhudi za upatanishi na kuzuia mpango wa usitishaji mapigano. Tuhuma ambazo zimekanushwa na serikali mjini Tel-Aviv.