1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yauwa watu 25 katika shule Gaza

4 Agosti 2024

Wapalestina wasiopungua 25 wameuwawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya Israel kufanya mashambuzizi yaliyozilenga shule mbili mjini Gaza.

https://p.dw.com/p/4j67i
Mashambulio ya bomu Gaza na Israel
Miili ya Wapalestina ikiwasilishwa katika Hospitali ya al-Ahli Baptist baada ya shambulio la Israeli kwenye kambi ya wakimbizi ya Al-Shati na kitongoji cha Al-Daraj katika Jiji la Gaza, Gaza Juni 24, 2024.Picha: Dawoud Abo Alkas/AA/picture alliance

Ripoti iliyotolewa na shirika rasmi la Habari la Palestina la WAFA imesema Shule hizo zilikuwa zikiwahifadhi watu waliolazimika kuyahama makazi yao katika mzozo unaoendelea kwenye ukanda huo.

Kwa upande wake jeshi la Israel limesema mashambulizi hayo ya Jumapili yaliwalenga wanamgambo wa Hamas waliokuwa wakiendesha shughuli zao karibu na eneo hilo zikiwa ni pamoja na kufanya mashambulizi dhidi ya Israel.

Mashambulizi hayo yaliyolenga shule ni kando ya mengine yaliyoripotiwa kufanywa na Israel ya mapema leo yaliyowauwa watu18 mjini Gaza wakiwemo wanne ambao walikuwa wamejihifadhi katika hema la kambi moja ya wakimbizi iliyo kwenye eneo la hospitali.