1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mashambulizi ya Israel yauwa takriban Wapalestina 100 Rafah

12 Februari 2024

Mashambulizi ya Israel ya kuamkia leo Jumatatu, katika mji wa Kusini mwa Gaza wa Rafah yameuwa takriban watu 100.

https://p.dw.com/p/4cIWx
Ukanda wa Gaza | Mashambulizi ya anga Rafah
Moshi ukifuka Rafah kufuatia mashambulizi ya Israel.Picha: SAID KHATIB/AFP

Taarifa hizo zimetolewa na wizara ya afya ya Gaza inayoongozwa na kundi la Hamas. Jeshi la Israel limetowa taarifa leo likisema mateka wawili waliokuwa mikononi mwa Hamas wamekombolewa katika operesheni hiyo.

Taarifa ya jeshi imesema  Fernando Simon Marman mwenye umri wa miaka 60 na Louis Har mwenye umri wa miaka 70 ni miongoni mwa watu waliotekwa nyara na kundi la Hamas Oktoba 7 katika eneo la Kibbutz Nir Yitzhak. Wote wawili wako katika hali nzuri kiafya.

Israel pia imesema  kiasi mateka 130 bado wanashikiliwa Gaza ingawa 29 wanafikiriwa huenda wamekufa. Jana kundi la Hamas lilisema mateka wawili wameuwawa kufuatia mashambulio ya Israel na wengine wanane wamejeruhiwa.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW