1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya Israel yapiga maghala ya makombora Syria

16 Desemba 2024

Shirika la kufuatilia hali ya vita nchini Syria, lenye makao yake nchini Uingereza, limesema mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel mapema leo, yamelenga maghala ya kuhifadhi makombora.

https://p.dw.com/p/4oC86
Mashambulizi ya ndege ya Syria
Israel imekuwa ikiishambulia kile ilichosema ni maeneo ya kijeshi ndani ya SyriaPicha: DELIL SOULEIMAN/AFP/Getty Images

Shirika hilo limesema mashambulio hayo ndio mabaya zaidi kufanywa na Israel ndani ya Syria tangu mwaka 2012. Israel imekuwa ikiishambulia kile ilichosema ni maeneo ya kijeshi ndani ya Syria baada ya kuangushwa utawala wa Bashar al Assad.

Soma pia: Israel yadhamiria kuongeza idadi ya watu eneo la Milima ya Golan

Jeshi la nchi hiyo pia limekalia eneo la usalama la mpakani na Syria,hatua inayokosolewa huku Israel ikishutumiwa kwa kukiuka makubaliano ya kusitisha vita ya mwaka 1974.

Wakati huo huo ubalozi wa Marekani mjini Damascus umewashauri raia wake waondoke Syria kutokana na hali ya usalama kuendelea kuwa tete na kutotabirika.