1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel: Raia karibu 50,000 waondoka kaskazini mwa Gaza

9 Novemba 2023

Jeshi la Israel limesema karibu raia 50,000 jana Jumatano wamelikimbia eneo la kaskazini mwa Gaza na kuelekea kusini katikati ya mzozo unaozidi kutokota.

https://p.dw.com/p/4YahY
Moto ukiwaka baada ya shambulizi la kombora la Israel katikati ya mzozo unaoendelea kati yake na kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza
Moto ukiwaka baada ya shambulizi la kombora la Israel katikati ya mzozo unaoendelea kati yake na kundi la Hamas kwenye Ukanda wa Gaza Picha: Israel Defense Forces/Handout via REUTERS

Msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari amesema wamewao wakazi hao wakiondoka na kuongeza kuwa wamechukua hatua hiyo kwa kuwa wameona Hamas imekwishapoteza udhibiti katika eneo hilo na kukimbilia kusini kuliko na usalama.

Katika hatua nyingine, Italia imesema imepeleka meli yenye hospitali karibu na eneo la maji la Gaza ili kusaidia kuwatibu wahanga wa mzozo huo, hii ikiwa ni kulingana na waziri wa ulinzi Guido Crosseto.

Meli hiyo itasimama Cyprus kabla ya kuelekea kwenye eneo lililo karibu zaidi na Ukanda wa Gaza, na majeruhi watapelekwa kwenye meli hiyo na kutibiwa kisha watarudishwa Gaza.