1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mashambulizi ya anga ya Israel yawaua takriban 24 mjini Gaza

25 Juni 2024

Maafisa wa afya katika Ukanda wa Gaza, wamesema jeshi la Israel limewauwa Wapalestina 24 katika mashambulizi matatu tofauti ya ndege mjini Gaza huku vifaru vikiingia ndani kabisa ya mji wa Rafah, kusini mwa Gaza.

https://p.dw.com/p/4hTnw
Vita vya Israel na wanamgambo wa Hamas
Moja ya vifaru vya jeshi vya Israel mjini RafahPicha: Amir Levy/Getty Images

Mashambulizi miwili kati ya hayo yalizilenga shule mbili katika mji wa Gaza na kusababisha vifo vya watu 14. Lingine lilishambulia nyumba moja eneo la Shati na kusababisha vifo vya watu 10.

Nyumba ya ebeo hilo la Shati inamilikiwa na familia iliyopanuka ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, ambaye anaishi Qatar, na shambulio hilo limemuuwa mmoja kati ya dada zake pamoja na ndugu wengine pia.

Ndugu wa mateka wa Gaza wasema vita havitaisha bila kuwachia kwao

Haniyeh, ambaye anaongoza diplomasia ya Hamas na ndiye uso wa umma wa kundi hilo ambalo limekuwa likiongoza Gaza, amepoteza jamaa zake wengi katika mashambulizi ya anga ya Israel tangu Oktoba 7, wakiwemo wanawe watatu.