1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Maseneta wa Marekani wachapisha rasimu ya mpango wa usalama

5 Februari 2024

Maseneta nchini Marekani wamechapisha Jumapili rasimu ya mpango ambayo huenda ukawezesha upatikanaji wa msaada mpya wa mabilioni ya dola kwa Ukraine na Israel pamoja na kuimarisha sheria za mipaka ya Marekani.

https://p.dw.com/p/4c2OT
Bunge la Marekani-Capitol
Bunge la Marekani mjini Washington maarufu kama CapitolPicha: J. Scott Applewhite/AP Photo/picture alliance

Mpango huo unaofahamika zaidi kama "msaada wa ziada wa usalama" unajumuisha jumla ya dola bilioni 118.3, zikiwemo dola bilioni 60 za kuisaidia Ukraine kukabiliana na uvamizi wa Urusi, dola bilioni 14.1 kwa ajili ya Israel na dola bilioni 20.2 za kuimarisha usalama kwenye mipaka ya Marekani.

Soma pia: Zelensky kuwahutubia maseneta wa Marekani kufuatia msaada uliozuiliwa

Matarajio ya rasimu hiyo yenye kurasa 370 kuwa sheria bado ni hafifu kutokana na mivutano ya kisiasa. Rais Joe Biden amewatolea wito wabunge wa Republican kuunga mkono rasimu hiyo inayotarajiwa kujadiliwa Bungeni wiki hii.