1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marseille kupambana na Lazio, Frankfurt ligi ya Ulaya

Sekione Kitojo
31 Agosti 2018

Marseille ya  Ufaransa, ambayo ilikuwa  katika  fainali  ya  kombe la ligi  ya  Ulaya  msimu  uliopita, imewekwa  pamoja  na Lazio Rome na  Eintracht  Frankfurt  katika  kundi  gumu  la  ligi  ya  Ulaya.

https://p.dw.com/p/347Kk
Fussball Europa League Finale Pokal  - Olympique Marseille v Atletico Madrid
Picha: picture-alliance/Actionplus

Arsenal wamwekwa  katika  kundi  rahisi dhidi  ya  Sporting Lisbon, Qarabag  ya  Azerbaijan na Vorskla  ya  Ukraine. Klabu  nyingine  ya England   katika  kinyang'anyiro  hicho  cha  Ulaya, Chelsea, itacheza  na  PAOK Saloniki, BATE Borisov kutoka  Belarus  na Vidi ya  Hungary.

Fußball Europa League Arsenal - Atletico Madrid
Wachezaji wa Arsenal London waliovalia sare nyekundu na nyeupe na Atletico Madrid (sare za njano )wakipambana kuwania mpira katika mchezo wa ligi ya mabingwa msimu uliopita 2017/18Picha: Reuters/E. Keogh

Mabingwa  wa  Scottland  Celtic  iko  katika  kundi  ambalo linajumuisha  klabu  mbili  zinazodhaminiwa  na  kampuni  ya  Red Bull, Salzburg, iliyoondolewa  katika awamu ya  nusu  fainali  msimu uliopita, RB Leipzig, pamoja  na  Rosenbourg ya  Norway.

Rangers, inakumbana  na  kizingiti  kigumu kusonga  mbele  wakati ikirejea  katika  mapambano  ya  Ulaya  dhidi  ya  Villarreal  ya Uhispania, Rapid Vienna  na  Spartak Moscow.

Dudelange, klabu  ya  kwanza  kutoka  Luxembourg  kufika awamu ya  makundi  katika  kinyang'anyiro  hicho, wamepewa  safari ya kwenda  San Siro kucheza  na  AC Milan, ambao  wameshinda mataji  manane  ya  Ulaya, na  pia  watakumbana  na  Real Betis na Olympiakos.

Antoine Griezmann , ambaye  alifunga  mabao  mawili  katika  fainali ya  msimu  uliopita  wakati  Atletico Madrid  ilipoishinda  Marseille kwa  mabao 3-0, alitajwa  kuwa  mchezaji  bora  wa  ligi  ya Ulaya msimu  uliopita.

Europacup - Marseille Atletico
Antoine Griezmann akishikilia kombe la ligi ya Ulaya pamoja na mchezaji mwenzake wa Atletico Madrid Diego GodinPicha: picture-alliance/AP Photo/C. Ena

Griezmann mshindi  wa  taji  la  dunia  akiwa  na  Ufaransa, pia alimaliza  akiwa  wa  nne  katika  tuzo  ya  mchezaji  bora  wa  EUFA msimu  uliopita tuzo  zilizotangazwa  jana  Alhamis  na  mchezaji kutoka  Croatia Luka Modric ndie  aliyeshinda  tuzo  hiyo, mshindi wa  fainali  ya  kombe  la  mabingwa  wa  Ulaya  na  makamu  bingwa wa  kombe  la  dunia. Duru  ya  kwanza  ya  michezo  hiyo itafanyika Alhamis , Septemba 20.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Iddi Sssessanga