1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yazindua luteka ya kijeshi na Mataifa ya Afrika

2 Machi 2023

Marekani imeanzisha hapo jana nchini Ghana mpango wake wa kila mwaka wa kutoa mafunzo ya kukabiliana na ugaidi kwa vikosi vya kiafrika.

https://p.dw.com/p/4O9RJ
Das gepanzerte Fahrzeug Stryker  der US Armee
Picha: Jung Yeon-je/AFP

Marekani inashirikiana na Mataifa ya Magharibi katika kutoa mafunzo hayo kwa wanajeshi kutoka mataifa yote ya Afrika.

Mpango huo unaofahamika kama "Flintlock " umeanzishwa katika kambi ya kijeshi ya Daboya kaskazini mwa Ghana na unalenga kuimarisha ulinzi wa mpakani na kupambana dhidi ya makundi yenye itikadi kali za Kiislamu ambayo yanazidi kutanuka maeneo ya kusini.

Vitendo vya makundi hayo vilivyosababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao, vimekuwa vikiripotiwa katika nchi za Mali, Niger, Burkina Faso, Benin, Togo na Ivory Coast.