1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Marekani yaweka vikwazo vipya dhidi ya taasisi za Sudan

1 Juni 2023

Wizara ya fedha ya Marekani imeweka vikwazo vipya vinavyozilenga taasisi za nchini Sudan. Tovuti ya wizara hiyo imesema imetoa vibali jumla vinavyoruhusu mashirika kadhaa ya msaada kufanya kazi nchini Sudan.

https://p.dw.com/p/4S4lG
USA Forderung nach Intervention im Sudan in Washington
Picha: AFP

Mapema leo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alikuwa ameonya kwamba nchi yake inaweza kuwachukulia hatua viongozi wa makundi yanayopigana nchini Sudan baada ya kuvunjika kwa makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani na Saudi Arabia.

Mwanadiplomasia huyo wa Marekani  hakubainisha wazi ikiwa hatua hizo zitawalenga majenerali wanaoongoza makundi hasimu katika mzozo wa Sudan.

Wakati huo huo duru kutoka Sudan zimearifu kuwa watu 18 wameuawa katika shambulizi la anga lililolipiga soko moja mjini Khartoum leo Alhamisi. Na Umoja wa Mataifa umesema kuwa idadi ya raia wa Sudan waliokimbilia nchini Chad imepindukia watu 100,000.