1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMali

Marekani yaweka vikwazo kwa baadhi ya maafisa wa Mali

25 Julai 2023

Marekani imemuwekea vikwazo Waziri wa Ulinzi wa Mali, Sadio Camara, na maafisa wengine wawili iliowatuhumu kwa kulisadia kundi la mamluki la Urusi la Wagner, ambalo imesema linafanya kazi kama jeshi la wakala wa Kremlin.

https://p.dw.com/p/4UNNH
China | US Außenminister Blinken in China
Picha: Ichiro Ohara/The Yomiuri Shimbun/AP/picture alliance

Katika taarifa hapo jana, wizara ya fedha ya Marekani iliwawekea vikwazo waziri huyo, mkuu wa jeshi la anga,  Alou Boi Diarra, na naibu wake, Adama Bagayoko, kwa kusaidia kuongezeka shughuli za kundi la Wagner nchini Mali .

Soma pia:HRW:Wanajeshi Mali,Wagner wamefanya mauaji ya raia kiholela

Brian E. Nelson, katibu wa wizara ya fedha anayehusika na masuala ya ugaidi na ujasusi wa kifedha, amesema maafisa hao wamewaweka watuwa nchi hiyo katika hatari ya kundi la Wagner na unyanyasaji wa haki za binaadamu huku wakitoa njia ya ufujaji wa rasilimali za nchi yao kwa manufaa ya shughuli za kundi hilo nchini  Ukraine.