1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yauwa wanamgambo watatu Somalia

24 Januari 2024

Jeshi la Marekani limesema lilifanya mashambulizi ya anga nchini Somalia mwishoni mwa juma, ambapo wanamgambo watatu wa kundi la Al-Shabaab lenye mafungamano na kundi la Al-Qaeda waliuawa.

https://p.dw.com/p/4bcSN
Somalia Al-Shabaab
Wanamgambo wa Al-Shabaab kwenye picha iliyopigwa kwenye viunga vya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, mwaka 2011.Picha: picture alliance / AP Photo

Kamandi ya Marekani inayohusika na Afrika yenye makao yake makuu mjini Stuttgart, Ujerumani, imesema katika taarifa yake kwamba mashambulizi hayo yalifanyika kutokana na ombi la serikali ya Somalia.

Mashambulizi hayo yalifanywa kwenye eneo la ndani, karibu kilomita 35 kaskazini mashariki mwa mji wa bandari wa Kismaiyo.

Kundi la Al-Shabaab limekuwa likiendesha uasi kwa takribani miaka 16 dhidi ya serikali ya Somalia inayoungwa mkono na nchi za magharibi na vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika.

Wanamgambo hao pia wamefanya mashambulizi makubwa katika nchi jirani ya Kenya.