1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yatoa ahadi ya dola bilioni 3 kwa mazingira

2 Desemba 2023

Makamu wa Marekani Rais Kamala Harris ameuleza mkutano wa COP28 wa Dubai kwamba Marekani itachangia dola bilioni 3 kwa mfuko wa mabadiliko ya tabia nchi duniani ikiwa ni ahadi ya kwanza ya nchi hiyo tangu 2014.

https://p.dw.com/p/4Zi2A
Sarah bint Yousef Al Amiri und Kamala Harris
Sarah bint Yousef Al Amiri na Makamo wa Rais wa Marelani Kamala Harris wakiwa DubaiPicha: Amr Alfiky/REUTERS

Makamo huyo wa rais aliongeza kwa kusema Marekani inaonyesha kwa vitendo jinsi ulimwengu unavyoweza na kwa lazima kukabiliana na shida hii ya mabadiliko ya tabia nchi. Kiwango hicho kipya cha fedha ambacho lazima kiidhinishwe na Bunge la Marekani, kitaingia katika Mfuko wa kukabiliana na madhila yamabadiliko ya tabia nchi duniani kwa kifupi,(GCF), ambao uliundwa mwaka wa 2010.Mchango wa mwisho wa Marekani katika mfuko huo wa mataifa yanazoendelea ulitolewa chini ya Rais wa wakati huo Barack Obama, ambaye alitoa dola bilioni 3 mwaka 2014. Kabla ya tangazo hilo la Marekani, dola bilioni 13.5 zilikuwa zimeahidiwa kwa mfuko huo wa GCF.