1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yasimamisha misaada ya chakula nchini Ethiopia

Daniel Gakuba
8 Juni 2023

Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa, USAID limesimamisha msaada wa chakula kwa Ethiopia, lisema msaada huo hauwafikii walengwa.

https://p.dw.com/p/4SLYE
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alipozuru ghala ya chakula cha misaada inayotolewa na shirika la maendeleo la Marekani, USAID, lililopo Addis Ababa, Ethiopia.
Marekani ndi mfadhili mkubwa kabisa wa Ethiopia katika sekta ya msaada wa kibinadamu.Picha: Tiksa Negeri/REUTERS

Msemaji wa shirika hilo ameeleza katika taarifa, kwamba USAID na serikali ya Ethiopia wamegundua kuwapo kwa hila iliyoratibiwa, ya kuubadishia njia msaada wa chakula ili usiwafikie wenye mahitaji. Ingawa msemaji huyo hakuwataja wahusika, nyaraka za muungano wa mashirika ya msaada zinawatuhumu maafisa wa tawala za mikoa na vikosi vya jeshi kujinufaisha na msaada huo.

Marekani ndiyo mfadhili mkubwa kabisa wa Ethiopia katika sekta ya msaada wa kibinadamu, ambapo inawasaidia watu wapatao milioni 20 wanaokumbwa na njaa kutokana na ukame na pia vita katika jimbo la Tigray ambavyo vilimalizika hivi karibuni.