1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema yafuatilia kwa karibu kinachoendelea China

29 Novemba 2022

Rais Joe Biden wa Marekani anafuatilia vurugu zinazoendelea China, zikihusisha waandamanaji wanaodai kufikishwa mwisho hatua za kufungwa kwa shughuli za maisha zinazolenga kuzuia usambaaji wa virusi vya Corona.

https://p.dw.com/p/4KDRq
Taiwan | Mahnwache für die Proteste in China
Picha: Yuchen Li/DW

Waandamanaji pia wanadai uhuru zaidi wa kisiasa.Ikulu ya Marekani imesema rais Biden anafuatilia kinachoendelea China katika wakati ambapo pia ndani ya Marekani yamezuka maandamano ya kuonesha mshikamano na  waandamanaji nchini China.

Msemaji wa baraza la usalama la Marekani John Kirby amewaambia waandishi habari jana Jumatatu kwamba wanatazama kinachojitokeza kutoka China lakini rais Biden hatozungumza kwa niaba ya waandamanaji duniani isipokuwa waandamanaji watajipazia sauti wenyewe.

soma zaidi: China: Maandamano yaenea kupinga sera kali za kudhibiti UVIKO

Ingawa ametilia mkazo kwamba Marekani inaunga mkono haki ya waandamanaji.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani jana ilisema sera ya China kuhusu kuzuia  virusi vya Corona imepindukia mipaka na kwamba itakuwa vigumu kwa nchi hiyo kudhibiti usambaaji virusi hivyo kwa kutumia mkakati wake huo.

Chanzo: afp
 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW