1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yasema inataka kuizuia Iran, si vita

22 Mei 2019

Wabunge wa Marekani wamesema maafisa wa Marekani wamelirifu bunge kuhusu mvutano na Iran na kuwashawishi kwamba serikali inataka kuzuia uchokozi wa Iran na si kuliingilia kijeshi taifa hilo la Kiislamu. 

https://p.dw.com/p/3IrpX
USA Verteidigungsministerin von der Leyen in Washington
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Baada ya kikao cha faragha cha wabunge mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya nje Eliot Engel amewaambia waandishi wa habari kwamba wanadhani wanajaribu kupunguza hofu inayoletwa na vita vya maneno, na kusema maafisa hao wamejaribu kuwapa mtizamo huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo, mwenyekiti wa umoja wa wakuu wa utumishi, Jenerali Joseph Danford pamoja na kaimu waziri wa ulinzi Patrick Shanahan waliwaarifu wabunge, wa Republican na Democrats waliotaka taarifa zaidi kuhusu kuongezeka kwa hali ya wasiwasi na Iran.

Na baada ya kikao hicho cha ndani, kaimu waziri Shanahan akawaambia waandishi wa habari kuhusu kile walichoafikiana, "Tulikuwa na mazungumzo mazuri sana na baza la wawakilishi na baraza la Seneti. Tumesikia maoni yao wakitaka mazungumzo zaidi na kuzungumza na umma wa Marekani, na tumekubali kufanya zaidi ya hayo. Leo, nimaweleza kuhusu kile ambacho wizara ya ulinzi imekuwa ikifanya tangu Mei 3 tulipopata taarifa za kuaminika za kiintelijensia kuhusu vitisho dhidi ya maslahi yetu huko Mashariki ya Kati na majeshi ya Marekani".

USA verkündet Ende der Strafzölle auf Stahl und Aluminium
Wabunge w Democrats wana wasiwasi kuhusu mabadiliko ya ghafla ya sera za Trump kuelekea IranPicha: Getty Images/AFP/S. Loeb

Maafisa hao waliliarifu bunge, wakati maswali yakiongezeka kuhusu maneno makali anayoyatumia rais Donald Trump kuhusu Iran pamoja na mabadiliko ya ghafla ya sera zake kuelekea ukanda huo.

Kumekuwa na hisia tofauti baada ya kikao hicho cha faragha.

Wademoctrats wenye wasiwasi kuhusu hali hiyo walitafuta mawazo kutoka upande mwingine walipokutana na maafisa wa serikali ya rais Barack Obama, mkurugenzi wa zamani wa shirika la kijasusi, CIA, John Brennan na Wendy Sherman aliyeuandaa mkataba wa nyuklia wa Iran.

Mrepublican, Seneta Mitt Romney alisema hatua iliyochukuliwa na serikali ya Trump iko sahihi kabisa na inatuma ujumbe kwamba ikiwavamia watu wake, Marekani itajibu. 

Ruben Gallego, mwakilishi wa Democrats na veterani wa vita vya Iraq, alisema kile alichokisikia kinadhihirisha kwamba serikali ya Trump haitarudi na kujadiliana na bunge kuhusiana na hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi ya Iran.

WaDemocrats wana wasiwasi kwamba serikali huenda ikasalia kwenye ridhaa ya kwenda vitani iliyodumu kwa takriban miaka 20 badala ya kuomba upya kibali cha bunge. 

Ingawa Trump anaonyesha kuwa tayari kufanya mazungumzo na Iran, rais wa taifa hilo, Hassan Rouhani na kiongozi wa juu Ayatollah Khamenei wamesema hawako tayari kufanya hivyo.