1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri wa biashara wa Marekani azuru China kwa siku nne

27 Agosti 2023

Waziri wa biashara wa Marekani Gina Raimondo amewasili nchini China hii leo kwa ziara ya siku nne inayolenga kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya mataifa hayo yenye nguvu kubwa kiuchumi ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4VciV
Pichani ni waziri wa biashara wa Marekani Gina M. Raimondo, anayekwenda China kwa ajili ya mazungumzo ya kuimarisha uhusiano wa biashara
Marekani inaangazia namna itakavyopata suluhu ya mivutano ya mara kwa mara na ChinaPicha: Alex Edelman/CNP/MediaPunch/picture alliance

Waziri huyo wa biashara Gina Raimondo alimweleza rais Joe Biden siku ya Alhamisi alipozungumza naye juu ya ziara hiyo na ujumbe unaolenga kupunguza mivutano na China.

Amesisitiza kwamba anataka kuwa na mahusiano thabiti ya kibiashara na China na msingi wa hilo ni mawasiliano ya mara kwa mara.

Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng aliyekutana na Raimondo wiki iliyopita amesema China inataka kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote.

Soma pia: Uhusiano wa Marekani na China wachukua mwelekeo mpya