1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yapendekeza kusitishwa mapigano kwa muda Gaza

20 Februari 2024

Marekani imependekeza rasimu pinzani ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalotaka kusitishwa kwa muda kwa mapigano katika vita vya Israel na Hamas.

https://p.dw.com/p/4cb1J
Idadi ya vifo inazidi kuongezeka Gaza
Israeli inaendelea na operesheni yake ya kuyapiga maeneo ya kusini mwa GazaPicha: MOHAMMED SALEM/REUTERS

Pia linapinga operesheni kubwa ya ardhini ya mshirika wake Israel katika mji wa Rafah. Hatua hiyo inajiri baada ya Marekani kuashiria kuwa itatumia kura yake ya turufu leo kupinga azimio lililotayarishwa na Algeria - likitaka kusitishwa maramoja kwa mapigano.

Marekani inahofia kuwa rasimu hiyo inaweza kuhujumu mazungumzo kati ya Marekani, Misri na Qatar ambayo yanalenga kufikia makubaliano ya kuwekwa chini silaha katika vita hivyo na kuwachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Israel inapanga kuvamia Rafah, ambako Wapalestina milioni moja kati ya milioni 2.3 wa Ukanda wa Gaza wamekimbilia huko kutafuta hifadhi, hatua inayozusha wasiwasi wa kimataifa. Hii ni mara ya pili tangu shambulizi la Oktoba 7 kwa Washington kupendekeza azimio la Baraza la Usalama kuhusu Gaza. Urusi na China zilipiga kura ya turufu kupinga azimio la kwanza mwishoni mwa Oktoba.