1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yamuua kamanda wa Kataib Hizbullah

8 Februari 2024

Jeshi la Marekani limesema limemuua kamanda wa kundi la Kataib Hezbollah linaloungwa mkono na Iran nchini Iraq.

https://p.dw.com/p/4c9u3
Irak | Baghdad, Kataib Hizbullah
Gari lililoshambuliwa na kombora la Marekani na kumuuwa kamanda wa kundi la Kataib Hizbullah nchini Iraq.Picha: Hadi Mizban/AP Photo/picture alliance

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, kamanda huyo ndiye aliyekuwa akipanga mashambulizi dhidi ya wanajeshi wake kwenye ukanda wa Mashariki ya Kati. 

Taarifa ya jeshi la Marekani imesema vikosi vyake vilifanya shambulizi hilo nchini Iraq, ikijibu mashambulizi dhidi ya wanajeshi wake na kumuua kamanda huyo, ambaye halikumtambulisha.

Taarifa hiyo aidha imesema hakukuwa na raia aliyeathirika na shambulizi hilo, ingawa vyanzo vingine vinasema watu watatu waliuawa.

Vyanzo viwili vya jeshi, vilipozungumza kwa sharti la kutotambulishwa vimemtaja kamanda huyo kuwa ni Abu Baqir al-Saadi, aliyeuawa baada ya droni kushambulia gari yake mashariki mwa Iraq.