1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Marekani yamtaka Modi kusisitiza juu ya uadilifu wa Ukraine

9 Julai 2024

Marekani imetoa wito kwa waziri mkuu wa India Narendra Modi kusisitiza kuhusu uadilifu wa eneo la Ukraine wakati alipokutana na Rais Vladimir Putin nchini Urusi, mkesha wa mkutano wa kilele wa NATO mjini Washington

https://p.dw.com/p/4i23T
Waziri mkuu wa India Narendra Modi (kushoto) akutana na Rais wa Urusi Vladimir Putin wakati wa mkutano usio rasmi katika makazi ya serikali ya Novo-Ogarevo nje ya Urusi mnamo Julai 8, 2024
Waziri mkuu wa India Narendra Modi (kushoto) akutana na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Sergei Bobylev, Sputnik, Kremlin Pool Photo/AP/picture alliance

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Matthew Miller, amewaambia waandishi habari kwamba wanaihimiza India, kama wanavyofanya kwa nchi yoyote inayoshirikiana na Urusi, kuweka wazi kwamba azimio lolote la mzozo nchini Ukraine linapaswa kuheshimu Mkataba wa Umoja wa Mataifa pamoja na uadilifu na uhuru wa Ukraine.

India ni mshirika wa kimkakati wa Marekani

Miller ameongeza kuwa India ni mshirika wa kimkakati wa Marekani wanaoshirikiana nayo katika mazungumzo ya wazi na hilo linajumuisha wasiwasi wao juu ya uhusiano wake na Urusi.

Soma pia:Modi kuelekea Moscow

Hata hivyo Miller amesema kuwa hakufahamu kuhusu mazungumzo maalum naIndia kuhusu ziara ya Modi nchini Urusi.