1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yaionya RSF dhidi ya kuishambulia Darfur

2 Novemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amewaonya wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support Forces RSF dhidi ya kufanya shambulizi kubwa" katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini wa El Fasher

https://p.dw.com/p/4YKWs
Kiongozi wa kundi la wanamgambo la RSF Jenerali Mohamed Hamdan Daglo
Kiongozi wa kundi la wanamgambo la RSF Jenerali Mohamed Hamdan DagloPicha: Ashraf Shazly/AFP

Katika taarifa Blinken amesema hatua hiyo itawaweka watu hao katika hatari kubwa. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ametoa wito wa pande zinazozana kusitisha mashambulizi zaidi na kuwajibika chini ya sheria ya kimataifa ya kiutu kuhusu raia.

Ingawa Marekani haikutaja chanzo cha taarifa yake, taarifa hiyo inatiliwa maanani kwa kuwa imetoka kwa jina la Blinken.

Marekani yatiwa wasiwasi na mashambulizi ya RSF

Tangu mwezi Aprili, vita hivyo kati ya wanamgambo wa Rapid Support Forces RSF wanaoongozwa na Jenerali Mohamed hamdan Daglo, na vikosi vya jeshi la Sudan vilivyo chini ya mkuu wa nchi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, vimesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 9 na kuwaacha watu milioni 5.6 bila makao.