1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani yakiri kutekwa mfanyabiashara wa madawa ya kulevya

10 Agosti 2024

Wafanyabiashara wawili wa madawa ya kulevya nchini Mexico walisafirishwa mwezi wa Julai hadi Marekani kukabiliana na mashitaka ya ulanguzi wa madawa hayo, lakini kila mmoja alifika kwa njia tafauti na mwenzake.

https://p.dw.com/p/4jJbo
Ismael "El Mayo" Zambada
Ismael "El Mayo" ZambadaPicha: Tv Azteca/La Nacion/Zumapress/picture alliance

Ubalozi wa Marekani nchini Mexico umesema mfanyabiashara mkubwa wa madawa ya kulevya na mtoto kiongozí wa makundi ya madawa hayo, Joaquim Guzman Lopez "El Chapo" alijisalimisha mwenyewe, huku mshirika mkubwa wa baba yake, Ismael "El Mayo" Zambada, akikamatwa kwa nguvu na kupelekwa Marekani.

Wote wawili wamekanusha tuhuma za kusafirisha madawa ya kulevya nchini Marekani na mawakili wao wametowa taarifa zinazokinzana juu ya kukamatwa kwao.

Soma zaidi: Mke wa 'El Chapo" Guzman aachiwa huru kutoka jela ya Marekani

Wakili wa Zambada amesema Guzman Lopez na watu sita waliovalia kijeshi walimteka mteja wake kwenye mji mkuu wa jimbo la Sinaloa nchini Mexico na kumpeleka nchini Marekani bila ridhaa yake.

Lakini wakili wa familia ya Guzman inasema haukuwa utekaji bali kujisalimisha kulikotokana na mazungumzo ya muda mrefu.

Mkasa huo wa mwezi uliopita umezusha mtafaruku kwenye mataifa ya Amerika Kusini, ambapo rais wa Mexico amewashutumu viongozi wenzake wa eneo hilo kwa kutokuwa na mashirikiano.