1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Marekani yaishtumu Urusi kwa kutishia wafanyikazi wake

29 Agosti 2023

Marekani imeishtumu Urusi kwa kujaribu kuwatisha wafanyikazi wa Marekani baada ya chombo cha habari cha serikali ya Urusi kuripoti kuwa, mfanyikazi wa zamani wa ubalozi wa Marekani ameshtakiwa kwa ujasusi.

https://p.dw.com/p/4VgJ9
ABW in Polen
Picha: Leszek Szymanski/EPA/dpa/picture alliance

Mfanyikazi huyo wa ubalozi anashutumiwa kwa kukusanya taarifa juu ya vita vya nchini Ukraine kwa niaba ya Marekani.

Shirika la habari la serikali ya Urusi TASS imeinukuu idara ya usalama ya Urusi FSB kuwa, Robert Shonov, raia wa Urusi aliwasilisha taarifa kwa wafanyikazi wa ubalozi wa Marekanimjini Moscow juu ya kampeni ya kuandikisha vijana kujiunga na jeshi nchini Urusi.

FSB imesema inapanga kuwahoji wafanyikazi wa ubalozi wa Marekani waliokuwa wakiwasiliana na Shonov, ambaye tayari amekamatwa tangu mwezi Mei.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Mathew Miller ameeleza kuwa, tuhuma dhidi ya Shonov, ambaye Marekani inasema aliajiriwa na kampuni iliyopewa kandarasi kwenye ubalozi wake, hazina ukweli wowote.