1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Kim Jong Un ametembelea viwanda vya silaha

14 Agosti 2023

Kiongozi wa Korea KaskaziniKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametembelea viwanda vikubwikiwa ni pamoja na kiwanda cha makombora ya kimkakati

https://p.dw.com/p/4V7qN
Nordkorea Führer Kim Jong-un bei einer Inspektion großer Munitionsfabriken
Picha: Yonhap/picture alliance

Kulingana na shirika la habari la serikali, KNCA, kwenye ziara hiyo ya Kim, wiki iliyopita, alionyesha kuridhishwa na namna kiwanda hicho kilivyojiimarisha katika kutengeneza silaha hizo za kimkakati, pamoja na kuongeza uwezo wa uzalishaji.Hii ni ziara ya karibuni zaidi katika msururu wa ziara zake kwenye viwanda vya kijeshi.ambako alihimiza uzalishaji wa kiwango kikubwa cha silaha.Marekani imekuwa ikiishutumu Korea Kaskazini kwa kuipatia silaha Urusi wakati huu inapopambana na Ukraine, na mwezi uliopita ilisema ilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya mahusiano ya mataifa hayo mawili.