1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroYemen

Marekani yaharibu droni nane za waasi wa Houthi nchini Yemen

19 Juni 2024

Jeshi la Marekani limesema limeharibu vifaa vya rada na droni nane za kundi la waasi wa Kihouthi katika muda wa saa 24 zilizopita.

https://p.dw.com/p/4hDxO
Yemen Sanaa | Huthi
Wapiganaji wa kundi la Houthi wakiendesha gari wakiwa mji mkuu wa Sana'a, Yemen, 03 Juni 2024.Picha: Yahya Arhab/EPA

Kamandi Kuu ya Mashariki ya Kati ya jeshi la Marekani CENTCOM imesema katika taarifa kuwa, hakukuwepo majeraha yoyote au uharibifu wa meli za mizigo katika oparesheni hiyo.

Wahouthi wamekuwa wakizishambulia meli katika bahari ya Sham na ghuba ya Aden tangu Novemba mwaka 2023, katika kile wanachosema ni kuonyesha mshikamano na Wapalestina.

Soma pia: Wahouthi waidungua droni ya Marekani

Mashambulizi hayo yamesababisha gharama ya bima kwa meli za mizigo kuongezeka maradufu na kupelekea kampuni nyingi za meli kutumia njia ndefu za kuzunguka bara la Afrika badala ya kuelekea Bahari ya Shamu na Mfereji wa Suez katika safari zao kutoka Asia kuelekea Ulaya.