1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yachapisha picha za puto la China lililodunguliwa

23 Februari 2023

Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon imechapisha picha inayoonesha kile maafisa wa Marekani wanachoshuku kilikuwa puto la ujasusi la China lililodunguliwa katika eneo la bahari ya Marekani mwanzoni mwa mwezi huu.

https://p.dw.com/p/4Ns9W
Chinas Spionageballon über den USA
Picha: Joe Granita/Zuma/IMAGO

Picha hiyo inaonesha puto hilo likielea katika anga ya Marekani mnamo Februari 3. Msemaji wa wizara hiyo, Sabrina Singh, alisema ukusanyaji wa mabaki ya puto hilo lililodunguliwa siku moja baada ya kuchukuliwa kwa picha hiyo, ulikamilika mwishoni mwa wiki iliyopita, na sasa yanachunguzwa na idara ya upelelezi ya FBI.

Soma pia:Biden kuzungumza na Rais Xi kuhusu puto la ujasusi

Tukio hilo lilizidi kuzorotesha uhusiano kati ya Marekani na China. Washington inaishtumu Beijing kutumia puto hilo kupeleleza miundombinu yake ya kijeshi. Lakini China imekanusha madai hayo, ikisema puto hilo lilikuwa la utafiti wa kiraia lililopoteza mwelekeo.