1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani na Uingereza zashambulia waasi wa Yemen

12 Januari 2024

Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi makubwa ya anga yaliyoyalenga maeneo yanayoshikiliwa na waasi nchini Yemen.

https://p.dw.com/p/4bA3v
Mzozo wa Mashariki Yemen | MAshambulizi ya Kijeshi dhidi ya Wahouthi.
Marekani na washirika wake wamefanya mashambulizi dhidi ya WahouthiPicha: US Central Command via X/REUTERS

Mashambulizi hayo yamefanyika mapema leo, baada ya wiki tano za mashambulizi yaliyotatiza shughuli katika Bahari ya Shamu, yaliyofanywa na waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran, ikiwa ni kuonyesha mshikamano na wapiganaji wa Hamas.

Televisheni ya waasi wa Kihouthi, Al-Masirah imetangaza kuwa mashambulizi hayo yameilenga kambi ya jeshi la anga, viwanja vya ndege na kambi ya kijeshi.

Soma pia: Iran yalaaniwa vikali katika kura ya Baraza la Usalama

Rais wa Marekani Joe Biden, amesema mashambulizi hayo yanalenga kuhakikisha shughuli katika Bahari ya Shamu zinafanyika kwa uhuru, na ameahidi kuchukua hatua zaidi iwapo itahitajika.

Iran imelaani mashambulizi hayo na imeonya kuwa yatachochea kukosekana kwa utulivu kwenye ukanda huo. Iran imesema pia mashambulizi hayo yanakiuka sheria ya kimataifa. Kundi la Hamas nalo limelaani vikali mashambulizi ya Marekani na Uingereza nchini Yemen.