1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJapan

Marekani na Japan zalenga kuimarisha ushirikiano wa kijeshi

28 Julai 2024

Wakuu wa ulinzi wa Japan na Marekani pamoja na wanadiplomasia wakuu wamekubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano wao wa kijeshi kwa kuboresha kamandi na udhibiti wa vikosi vya kijeshi vya Marekani nchini Japan.

https://p.dw.com/p/4ipyA
Waziri mkuu wa Japan  Fumio Kishida (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) wakiwa katika ikulu ya White House mnamo Januari 13,2023
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida (kushoto) na Rais wa Marekani Joe Biden (kulia)Picha: Mandel Ngan/AP Photo/picture alliance

Viongozi hao wa Marekani na Japan wameelezea tishio linaloongezeka kutoka China kama changamoto kubwa zaidi ya kimkakati.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken na waziri wa ulinzi Lloyd Austin, walijiunga na wenzao wa Japan, Yoko Kamikawa na Minoru Kihara, katika Kamati ya Ushauri ya Usalama waJapanna Marekani huko Tokyo, inayojulikana kama mazungumzo ya usalama ya "2+2" ambapo walisisitiza tena ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kufuatia kujiondoa kwa Rais Joe Biden katika uchaguzi wa urais wa Novemba.

Austin asema kuimarishwa kwa kamandi kutakuwa na mabadiliko muhimu kwa vikosi vya Marekani nchini Japan

Austin amesema kuimarishwa kwa kamandi hiyo kutakuwa mabadiliko muhimu zaidi kwa vikosi vya Marekani Japan  na mojawapo ya maboresho yenye nguvu zaidi katika uhusiano wa kijeshi wa nchi hiyo mbili katika muda wa miaka 70.