1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Muhimu kuepusha vita kamili Mashariki ya Kati

6 Agosti 2024

Marekani imesema inafanya juu chini kuepusha vita kamili katika Mashariki ya Kati. Hayo ni wakati Israel ikiiendelea kuwa katika hali ya tahadhari kwa uwezekano wa hatua ya Iran kulipiza kisasi.

https://p.dw.com/p/4jBFB
Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Evan Vucci/IMAGO/UPI Photo

Iran iliapa kuwa inayo haki ya kulipiza kisasi kwa mauaji ya wiki iliyopita ya kiongozi wa kisiasa wa kundi la Hamas Ismail Haniyeh.

Shambulizi la Haniyeh ambalo Israel haijalizungumzia moja kwa moja, lilijiri saa chache baada ya shambulizi la Israel mjini Beirut kumuuwa Fuad Shukr, mkuu wa kijeshi wa vuguvu la Hezbollah nchini Lebanon, linaloungwa mkono na Iran. 

Wizara ya afya ya Lebanon imesema mashambulizi ya anga ya Israel kusini mwa Lebanon, yamewaua watu watano. Duru za vikosi vya usalama vya Lebanon vimesema zimesema wapiganaji wanne wa Hezbollah ni miongoni mwa waliokufa.

Soma pia:Iran: Tunayo haki ya kuiadhibu Israel kufuatia mauaji ya Haniyeh

Nao wanamgambo wa Hezbollah wamesema walifanya leo mfululizo wa mashambulizi ya droni na makombora kaskazini mwa Israel. Hezbollah hata hivyo imeonya kuwa hatua yake inayosubiriwa pakubwa ya kulipiza mauaji ya kamanda wake mwandamizi wiki iliyopita bado haijafanywa.

Jeshi la Israel limesema droni kadhaa za adui ziligundulika zikiingia katika anga zake kutokea Lebanon na moja ikadunguliwa.