1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani kupeleka meli na ndege za kivita Mashariki ya kati

3 Agosti 2024

Marekani imesema itaimarisha uwepo wake wa kijeshi kwenye kanda ya Mashariki ya Kati kwa kupeleka meli na ndege za ziada za kivita ili kuwalinda wafanyakazi wa Marekani na kuilinda Israel.

https://p.dw.com/p/4j4oo
Marekani kupeleka meli zaidi za kivita, ndege za kivita Mashariki ya kati
Marekani kupeleka meli zaidi za kivita, ndege za kivita Mashariki ya katiPicha: Andrew Schneider/U.S. Navy photo/abaca/picture alliance

Marekani imesema itaimarisha uwepo wake wa kijeshi kwenye kanda ya Mashariki ya Kati kwa kupeleka meli na ndege za ziada za kivita ili kuwalinda wafanyakazi wa Marekani na kuilinda Israel katika wakati mvutano unaoongezeka katika eneo hilo.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imetoa tangazo hilo baada ya Iran na washirika wake wa kikanda kuapa kulipiza kisasi kufuatia mauaji ya kiongozi wa Hamas mjini Tehran na kamanda wa Hezbollah mjini Beirut, jambo linalozidi kuongeza hofu ya mzozo mkubwa wa Mashariki ya Kati.

Mapema wiki hii, Israel ilimuua kamanda wa Hezbollah Fuad Shukr huko Beirut siku ya Jumanne, hatua ambayo Israel  ilisema ilikuwa ni jibu la shambulizi la roketi lililolafanywa na kundi hilo wiki iliyopita kwenye milima ya Golan.

Saa chache baadaye, kiongozi wa Hamas,  Ismail Haniyeh aliuawa katika mji mkuu wa Iran, shambulio ambalo Israel bado imejizuia kulizungumzia hadi sasa.