1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Marekani: Kongo haijatoa maelezo kukamatwa kwa raia wetu

4 Juni 2024

Ubalozi wa Marekani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umesema mamlaka za Kinshasa hazikutoa ushirikiano wala maelezo kuhusu Wamarekani waliokamatwa kufuatia jaribio la mapinduzi mwezi uliopita.

https://p.dw.com/p/4gdlr
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix Tshisekedi
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Felix TshisekediPicha: DW

Familia moja iliwasilisha maombi ya usaidizi kwa ubalozi huo kwa lengo la kuthibitisha iwapo mtoto wao bado yupo hai.

Jeshi la Kongo lilitoa majina ya Wamarekani watatu wanaoshutumiwa kuwa na jukumu katika shambulio hilo la Mei 19,  lililoongozwa na mpinzani asiye maarufu nchini Kongo Christian Malanga ambaye aliuawa huku washirika wake kadhaa wakikamatwa.

Soma pia:Kongo yamtaja Mmarekani wa tatu aliyehusika jaribio la mapinduzi

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imesema moja ya vipaumbele vyake vya juu zaidi ni kutoa usaidizi kwa Wamarekani waliozuiliwa nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na kuwatembelea mara kwa mara ili kuwahakikishia huduma ya matibabu na kusaidia kutafuta wakili anayezungumza Kiingereza.