1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Marekani yatangaza vizuizi kwa baadhi ya watu wa Liberia

28 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametangaza vikwazo vya Visa za kusafiria kwa watu wanaodhoofisha demokrasia nchini Liberia, wakati taifa hilo likikaribia kufanya uchaguzi mwezi Oktoba.

https://p.dw.com/p/4WtAz
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antonya Blinken ametangaza vikwazo vya kusafiri dhidi ya baadhi ya watu wanaoodhoofisha usalama nchini Liberia
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antonya Blinken ametangaza vikwazo vya kusafiri dhidi ya baadhi ya watu wanaoodhoofisha usalama nchini LiberiaPicha: Mary Altaffer/AP Photo/picture alliance

Antony Blinken amesema kwenye taarifa iliyochapishwa na wizara yake kwamba sera ya vizuizi vya visa inawalenga baadhi ya watu ambao si wa serikalini. Hata hivyo haijaweka wazi ni watu wangapi watakaozuiwa kwenda Marekani chini ya vizuizi hivyo.

Taarifa hiyo imefafanua kwamba walengwa wa vizuizi hivyo ni wale wanaodhoofisha demokrasia kwa kufanya udanganyifu au wizi katika mchakato wa uchaguzi, kuchochea vurugu au kujihusisha katika shughuli nyingine yoyote kwa nia ya kuathiri matokeo ya uchaguzi wa Liberia.