1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maporomoko ya ardhi yaua watu zaidi ya 150 nchini Myanmar

Saleh Mwanamilongo
2 Julai 2020

Watu wasiopunguwa 150 wamepoteza maisha katika kisa cha maporomoko ya ardhi katika mgodi wa kuchimba madini ya jade, kaskazini mwa Mynamar.

https://p.dw.com/p/3ehRt
Watu wakibeba maiti baada ya maporomoko ya udongo kwenye mgodi wa jade,Myanmar.
Watu wakibeba maiti baada ya maporomoko ya udongo kwenye mgodi wa jade,Myanmar.Picha: Reuters/MYANMAR FIRE SERVICES

Watu wasiopunguwa 150 wamepoteza maisha katika kisa cha maporomoko ya ardhi katika mgodi wa kuchimba madini ya jade, kaskazini mwa Mynamar. Kulingana na vyanzo vya usalama, wachimba migodi wamesombwa na matope yaliyosababishwa na mafuriko. Mamlaka nchini Mynamar inasema kuwa zoezi la uokoaji linaendelea.

Hii ni idadi kubwa ya vifo kutokea nchini humo kutokana na majanga ya asili.

Miili 130 ya watu waliofariki dunia iliondolewa katikia matope, na zoezi la kuitafuta miili na watu walio hai limesitishwa kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

"Kufikia sasa tumepata jumla ya miili 113," idara ya Zima Moto iliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook. Kwenye ukurasa huo, picha zinaonyesha timu ya waokoaji wakipanda kwenye mlima uliojaa matope, kwenye korongo la Hpakant, karibu na mpaka wa China. Polisi inaelezea kwamba idadi ya vifo ingekuwa kubwa kabisa, ikiwa viongozi hawangetoa tahadhari kwa wachimba migodi kuondoka siku moja kabla ya tukio hilo.

Kila mwaka, wachimba migodi kadhaa wanaotafuta mawe ya thamani hufariki dunia katika ajali zinazosababishwa na mazingira magumu ya kazi, hasa wakati wa msimu wa mvua. Tukio kubwa la maporomoko ya ardhi lilitokea mwaka 2015 ambako watu zaidi ya mia moja walikufa. Maporomoko hayo yaliwauwa watu wengine 50 mwaka uliopita. Migodi ya madini ya jade hutoa kiwango kikubwa cha mawe ambayo watu nchini Myanmar huenda kutafuta mawe yenye thamani.