1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapigano yanaendelea Sudan huku wajumbe wakitafuta suluhisho

7 Mei 2023

Mapigano yameendelea katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum huku wajumbe wa pande zinazopigana wakiwa nchini Saudi Arabia kwa ajili ya mazungumzo juu ya kuumaliza mgogoro

https://p.dw.com/p/4R0OL
Sudan | Kämpfe in Khartum
Picha: AFP/Getty Images

Mapigano hayo kati ya pande mbili za jeshi la Sudan mpaka sasa yamesababisha vifo vya mamia ya raia na wengine maalfu wameshaikimbia nchi yao. Saudi Arabia na Marekani zinafanya juhudi kwa lengo la kusuluhisha mgogoro wa nchini Sudan. Hata hivyo wajumbe wa pande hizo mbili, kwenye mazungumzo ya mjini Jeddah wametamka wazi kwamba wao wanajadili juu ya suala la misaada kwa raia na siyo juu ya kuvimaliza vita.

Soma zaidi:HRW yalaani matumizi ya silaha za kivita maeneo ya raia Sudan

Kiongozi wa upande wa kikosi cha dharura, RSF Mohammed Hamdan Dagalo amesema anatumai kwamba lengo linalokusudiwa litafikiwa kwenye mazungumzo hayo la kutenga njia salama kwa ajili ya raia.