1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Mapigano yazuka mashariki mwa Kongo kati ya jeshi na M23

12 Julai 2024

Kumezuka mapigano leo mashariki mwa Kongo kati ya waasi wa M23 na wafuasi wa kundi moja la raia waliojihami lililo na mafungamano na jeshi la Kongo.

https://p.dw.com/p/4iEkx
DR Kongo | Kirumba-Kivu Kaskazini
Jeshi la Kongo wakipita eneo la Kirumba, Kivu KaskaziniPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Kumezuka mapigano leo mashariki mwa Kongo kati ya waasi wa M23 na wafuasi wa kundi moja la raia waliojihami lililo na mafungamano na jeshi la Kongo. Haya ni kwa mujibu wa vyanzo vya eneo hilo. Safari Bindu, msemaji wa mojawapo ya makundi hayo ya raia waliojihami ameliambia shirika la habari la Ufaransa kuwa waasi wa M23 walikivamia kijiji cha Nyange na ndipo mapigano yalipozuka na kusambaa katika vijiji vingine. Msemaji wa jeshi la Kongo eneo la Kivu Luteni Kanali Guillaume Ndjike - GIYOOM NJIIKE, hapo jana alililaumu jeshi la Rwanda kwa kufanya mashambulizi kadhaa katika maeneo walipo wanajeshi wa Kongo na makundi hayo ya raia waliojihami katika vijiji vya Nyange na Mpati. Haya yote yanafanyika baada ya Marekani wiki iliyopita kutangaza usitishwaji wa mapigano kwa kipindi cha wiki mbili. Waasi wa M23 wameuzingira walau mji wote wa Goma, ambao ndio mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini na kuwauwa watu kadhaa na kuwaacha mamia kwa maelfu wengine bila makao.