1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Milipuko na milio ya risasi yaendelea kurindima Khartoum

20 Aprili 2023

Milipuko na milio ya risasi imeendelea kurindima katika mji mkuu wa Sudan Khartoum wakati mapigano kati ya pande mbili hasimu za kijeshi yakionyesha dalili za kutosimamishwa kabla ya kumalizika mfungo wa Ramadhan.

https://p.dw.com/p/4QLaA
Sudan Khartum | Flucht Bewohner vor Kämpfen
Picha: AFP

Watu takribani 300 wameuawa tangu kuzuka kwa mapigano siku ya Jumamosi baina ya vikosi tiifu kwa mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan na naibu wake Mohamed Hamdan Daglo anayeongoza kikosi cha wanamgambo cha Rapid Support forces RSF. Stephane Dujarric ni msemaji wa Umoja wa Mataifa.

Mapigano hayo yameingia siku ya sita leo baada ya makubaliano mengine ya kusitisha machafuko kuvunjika jana Jumatano. Kikosi cha RSF kilisema awali kwamba wanajeshi wake "wataheshimu kikamilifu usitishaji mapigano" kuanzia saa 12 jioni siku ya jumatano kwa muda wa saa 24 kama lillivyofanya jeshi. Lakini mashuhuda wamesema milio ya risasi iliendelea kusikika Khartoum usiku.