1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mapendekezo ya Trump yaendelea kupingwa na Baraza la Seneti

Yusra Buwayhid
2 Februari 2017

Rais wa Marekani, Donald Trump, amefanikiwa pale Rex Tillerson, alipoidhinishwa kuwa waziri wa mambo ya nje. Lakini bado anakabiliana na upinzani mkali, ikiwamo pendekezo lake la Jaji wa Mahakama Kuu ya Marekani.

https://p.dw.com/p/2Wr8o
USA Präsident Donald Trump Telefonat mit Australiens Premierminister Malcolm Turnbull
Picha: picture-alliance/dpa/Pete Marovich/CNP/AdMedia

Rais Donald Trump amesema ikilazimika Waripublican wachukue hatua ya kubadilisha sheria za Baraza la Seneti ili uteuzi wake wa, Neil Gorsuch, kama jaji wa Mhakama Kuu uweze kuidhinishwa kwa wingi mdogo wa kura, badala ya kura 60 zinazohitajika kwa sasa ndani ya baraza hilo lenye wajumbe 100.

Wakati wa kampeni zake za urais, Trump aliahidi kuteua Jaji wa Mahakama Kuu anayepinga utoaji mimba na atakaefanya kazi ya kubadilisha sheria iliyohalalisha utoaji mimba nchini Marekani.

Makundi ya kupigania haki za wanaotaka kutoa mimba wamelikosoa pendekezo hilo la Trump, nakusema Gorsuch ni kitisho dhidi ya haki za uzazi za wanawake, oamoja na uamuzi wa kihistoria uliofanywa na Makama Kuu mwaka 1973 wa kuhalalisha utoaji mimba nchini kote.

Haijulikani bado kama maseneta wa upande wa Republican wenye wingi wa viti 52-48, watafanikiwa kuwashawishi maseneta wanane wanaowahitaji kutoka upande wa Wademocrat kumpitisha Gorsuch, kama jaji wa Mhakama Kuu.

USA Trump Ernennung Neil Gorsuch
Neil Gorsuch pendekezo la Trump kama jaji wa Mhakama Kuu ya MarekaniPicha: Reuters/K. Lamarque

Uteuzi wa Baraza la Mawaziri na Wizara ya Nje

Baraza la Seneti limemuidhinisha, Rex Tillerson, kama waziri wa mambo ya nchi za nje licha ya kuwepo wasiwasi kwamba ana uhusiano wa karibu na Urusi, wakati huo huo kamati ya Seneti imemuidhinisha Jeff Sessions, kama mwanasheria mkuu.

Kwa upande wa kuteua Baraza la Mawaziri, maseneta wa chama cha Republican walichelewesha kupiga kura ya kumuidhinisha Mkuu wa Shirika la Kulinda Mazingira aliyependekezwa na Trump, baada ya maseneta wa chama cha Democratic  kuugomea mkutano huo, wakisema Scott Pruitt, aliyependekezwa na Trump anatiliashaka sayansi ya mabadiliko ya tabianchi. Kamati ya seneti pia imemthibitisha Mwakilishi Tom Price, kuwa mkuu wa Idara ya Afya na Huduma za Binadamu na Steven Mnuchin kuwa katibu wa hazina.

Uteuzi mwengine unaokabiliwa na upinzani mkali ni dhidi ya mwanaharakati, Betsy DeVos kama waziri wa elimu baada ya Warepublican wawili kuapa kupiga kura dhidi yake. DeVos, ni bilionea na mfadhili mkubwa wa chama cha Republican ambaye kwa zaidi ya miongo miwili amekuwa akisaidia kusimamia shule zinazojitegemea wenyewe kwa msaada wa umma nchini Marekani.  Ni mojawapo ya uteuzi wa Trump ulio na utata na unaokabiliwa na upinzani mkali kutoka upande wa Wademocrat, vyama vya walimu pamoja na wanaharakati wanaopigania haki za kiraia. Uteuzi huo unaweza ukashindikana iwapo DeVos atakosa uungwaji mkono wa Mrepublican mmoja tu, na Wademocrat wote wakawa wamempinga. Lisa Murkowski, seneta wa jimbo la Alaska amesema, anaamini DeVos bado anahitaji kujifunza mengi kuhusu elimu ya uma.

Russland Putin überreicht "Orden der Freundschaft" an Tillerson
Rex Tillerson, Waziri mpya wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, akiwa na Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: picture alliance/dpa/K. Mikhail

Marufuku ya kusafiri

Chini ya thuluthi moja ya Wamarekani wanaamini kuwa amri ya rais, Donald Trump, ambayo kwa muda inazuwia  uhamiaji wa raia kutoka mataifa saba yenye Waislamu wengi, itaimarisha usalama nchini humo, kulingana na maoni ya raia yaliyokusanywa na shirika la habari la Reuters.

Aidha wataalamu wa haki za binaadamu wa Umoja wa Mataifa, wameonya kwamba wahamiaji wanaoomba hifadhi, wanaweza kukabiliana na mateso iwapo watanyimwa hifadhi. Vatican nayo imetoa wito wa kuzikubali tamaduni nyengine, ikikosoa uamuzi wa Trump wa kupiga marufuku kwa raia wa nchi saba kuingia nchini Marekani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema vikwazo vya kusafiri dhidi ya wahamiaji sio njia muafaka ya kuwalinda Wamarekani, na amemtaka Trump atengue amri hiyo haraka iwezekanavyo.

USA Donald Trump und Betsy DeVos
Betsy DeVos akiwa na Rais Donald TrumpPicha: Picture-Alliance/AP Photo/C. Kaster

Upinzani

Ilani iliyosainiwa na wafanyakazi 900 wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, ya kupinga mpango wa uhamiaji wa Trump ni mfano mmoja tu wa upinzani ulioenea dhidi ya Trump.

Na kwa upande wa bara la Ulaya, washirika wa karibu wa Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya wamekasirishwa na namna Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa Mei alivyomkumbatia Trump. Na wana hofu kwamba Uingereza, inajisogeza karibu mno na Trump kuelekea mchakato wa taifa hilo kujitoa katika Umoja wa Ulaya - Brexit.  

      

Mwandishi: Yusra Buwayhid/ape/rtre/ap/ 

Mhariri: Yusuf Saumu