1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Mapambano yazidi kuzizima mjini Khartoum

10 Mei 2023

Mapigano katika mji mkuu wa Sudan Khartoum yameongezeka leo pamoja na makabiliano makali na mashambulizi ya angani.

https://p.dw.com/p/4RA3D
Sudan Khartoum | Moshi ukionekana katika moja ya maeneo kwenye mji huo mkuu wa Sudan wakati kukiripotiwa mashambulizi zaidi Mei 10, 2023
Mji wa Khartoum bado unakabiliwa na hali tete kutokana na mapigano kati ya vikosi vya serikali na vikosi vya dharura vya RSF.Picha: Ahmed Satti/Anadolu Agency/picture alliance

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa pande mbili zinazohasimiana Sudan wakiendelea na mazungumzo nchini Saudi Arabia ya kufikiwa makubaliano ya kusitishwa mapigano na kupelekwa msaada wa kitu. Wakaazi wameripoti mapigano makali ya ardhini katika viunga vya mji mkuu Khartoum, kati ya jeshi na wanamgambo wa kikosi cha Rapid Support (RSF). Mapambano ya silaha nzito pia yameshuhudiwa kaskazini mwa Omdurman na mashariki mwa Bahri, miji miwili ambayo Mto Nile ndio umeitenganisha na Khartoum. Tangu jana, jeshi limekuwa likiyalenga maeneo ya miji mitatu, likijaribu kuwaondoa wanamgambo wa RSF ambao wamechukua udhibiti wa maeneo makubwa ya makaazi na maeneo ya kimkakati tangu machafuko hayo yalipoanza Aprili 15.