1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maonyesho ya filamu barani Afrika mjini Ouagadougou

oummilkheir3 Machi 2005

Maonyesho ya 11 ya filamu barani Afrika, kwa jina Fespaco yanaendelea hadi march tano ijayo katika mji mkuu wa Bourkina Faso Ougadougou.Waandalizi wa maonyesho hayo makubwa kabisa ya aina yake barani Afrika,wanasema mahitaji yamepindukia kilichopo safari hii.

https://p.dw.com/p/CHhJ

Filamu zaidi ya 340 zinaoonyeshwa kibiashara katika kipindi kizima cha FESPACO,pakiwepo zaidi ya vipanda 30 vya kutembeza biashara ya filamu za bara la Afrika. Kwa mara ya kwanza tangu maonyesho ya FESPACO yalipoanza mwaka 1983,mchapa filamu mashuhuri wa kutoka Senegal Ousmane Sembene,mkongwe miongoni mwa wakongwe wa fani hiyo barani Afrika,nae pia amefungua kibanda kuzitembeza filamu zake,kuanzia "La Fille Noire" au msichana mweusi aliyoiandaa katika mwaka 1966 hadi kufikia Moolaade ya mwaka jana.

Katika hotuba zao za ufunguzi,waziri wa utamaduni wa Bourkina fasso Mahamoudou Ouedraogo na mkuu wa FESPACO Baba Hama wamezungumzia kishindo kinachoikabili hatima ya filamu ya kiafrika.

"Vyenzo vya kukusanya fedha kwaajili ya kugharimia filamu za bara la Afrika vinapungua,kuna shida katika kuhakikisha usambazaji wa filamu zenyewe na miundo mbinu ya kutengeneza filamu katika nchi za kusini,ikikuwepo basi utakuta ni dhaifu.

Filamu 20 za kanda za muda mrefu,nne kati ya hizo ni za kutoka Burkina fasso na nne za Afrika kusini zinashindania Etalon d’or de Yennenga au kinyago cha dhahabu cha farasi dume.

Mbali na hizo kuna filamu ya Hassan Benjelloun wa Moroko kwa jina "Chambre Noire "The Black Room" inayozungumzia juu ya mateso katika jela za Moroko katika miaka ya 60 na 70.

Katika filamu aliyoitengeneza mwaka 2001 kwea jina "Jugement d’une Femme au Judgement of a Woman,Benjelloun anamulika jinsi haki za mwanamke zinavyokanyangwa nchini Moroko-filamu iliyowafumbua macho viongozi wa Moroko na kuanza kurekebisha sheria kuhusu wakinamama katika nchi hiyo ya kifalme .

Wasanii watatu wakike wanapigania pia nafasi ya kunyakua Etalon d’Or de Yennenga.Branwen Okpako Mnigeria anaeishi nchini Ujerumani na filamu yake kwa jina Valley of the Innocent,"La Nuit de la Verité au "The Night of Truth "ya Fanta Regina Nacro wa Burkina fasso na "Sous la Clarte de la Lune au Under the Moon Light iliyoandaliwa na Appoline Traore pia wa Burkina fasso.

Mkurugenzi wa FESPACO Baba Hama amesifu muamko wa wakinamama wafafanya filamu barani Afrika.Anasikitika lakini akisema katika jamii yetu ya kiafrika wanawake wachache tuu ndio wanaopata fursa ya kwenda shule.Anasema "Wanawake wengi wanalazimika kusalia majumbani,wachache ndio wanaopata fursa ya kwenda shule,kwa hivyo ni wachache pia wanaofanikiwa kuingia katika soko la filamu.

Okpako anahisi ufanisi wa wakinamama ni matokeo ya kubadilika mitazamo ya hali ya mambo barani Afrika.

Anasema tunanukuu:" hali namna ilivyo hivi sasa barani Afrika inahimiza suluhu,na wanawake ndio wenye tabia ya kupenda kusuluhusisha mambo."Mwisho wa kumnukuu.

Hakuna hadi wakati huu mwanamke yeyote aliyewahi kushinda zawadi katika maonyesho hayo ya Fespaco yanayofanyika kila baada ya miaka miwili.

Sherehe za ufunguzi wa maonyesho hayo ziligubikwa na mtafaruku mamia kadhaa ya watu walipokua wakisukumana kutaka kuingia katika uwanja wa maonyesho.Watu wawili waalipoteza maisha yao.