1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya wahariri juu ya kushambuliwa ubalozi wa Iran

Abdu Said Mtullya20 Novemba 2013

Pamoja na masuala mengine wahariri wanazungumzia juu ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Iran mjini Beirut na mazungumzo juu ya mpango wa nykulia wa Iran

https://p.dw.com/p/1ALEC
Ubalozi wa Iran mjini Beirut washambuliwa
Ubalozi wa Iran mjini Beirut washambuliwaPicha: Reuters

Na tunaanza na maoni ya gazeti la "Die Rheinpfalz" juu ya kushambuliwa kwa ubalozi wa Iran mjini Beirut. Mhariri wa gazeti hilo anasema kadhia hiyo inathibitisha kwamba vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria vinavuka mipaka ya nchi hiyo na kuzikumbuka nchi nyingine. Mhariri wa gazeti hilo anasema vita vya nchini Syria ni mapambano ya kimadhehebu.

Mhariri wa "Die Rheinpfalz" anatilia maanani kwamba wakati utawala wa Assad unapata ushindi katika uwanja wa mapambano,magaidi wa al-Qaeda wamejitokeza nchini Lebanon na kuushambulia ubalozi wa Iran, nchi inayomuunga mkono Assad.

Mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran

Mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran yanaendelea leo mjini Geneva. Na mhariri wa gazeti la "Nordwest" anauzingatia msimamo wa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu juu ya mazungumzo hayo na anasema kwamba wanasiasa na wadadisi wengi duniani wanamlaumu Waziri Mkuu Netanyahu kwa msimamo wake juu ya Iran. Hiyo si haki na vile vile ni dalili ya kutoyajua mambo.Yapasa kutambua kwamba Iran asilani haifikirii kuachana na mpango wake wa nyuklia. Itakuwaje ,Iran nchi yenye akiba kubwa kabisa ya mafuta duniani iseme kwamba inakusuduia kuzalisha nishati tu kwa kutumia nguvu za nyuklia.? Hapa inapasa kuuliza, kwa nini Iran inahitaji makombora ya masafa marefu na ya kati? Kwa hivyo tunaweza kuelewa kwa nini Waziri Mkuu wa Israel anataka mpango wa nyuklia wa Iran uzuiwe.

Hata hivyo mhariri wa"Berliner Zeitung" anakumbusha kwamba Israel pia inazo silaha za nyuklia, pia kutokana na msaada wa Ujerumani. Na kwa hivyo lingekuwa shauri zuri kama Netanyahu angelikuwa na msimamo wa utulivu.

Mazungumzo juu serikali ya mseto

Mhariri wa gazeti la "Neue Westfälische"anatoa maoni juu ya mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto nchini Ujerumani, baina ya chama kikuu cha upinzani,Social Demokratik na vyama vya kihafidhina vya CDU na CSU.Mhariri huyo anavinasihi vyama hivyo kwa kusema kwamba vyama hivyo vimeshinda uchaguzi, lakini havina sera mbadala kabisa ya zile za vyama vya upinzani .Ikiwa utafanyika uchaguzimpya,mizani haitabadilika sana. Hali hiyo itamlazimisha Kansela Merkel akisogeze chama chake cha CDU karibu na sera za mrengo wa shoto.Katika muktadha huo mjadala juu ya utambulisho wa chama cha CDU utapamba moto katika chama hicho. Si rahisi kutabiri iwapo hatimaye chama cha CDU cha Kansela Merkel kitaibuka kuwa na uzito zaidi katika serikali ya mseto.

Mwandishi:Mtullya Abdu/Deutsche Zeitungen .

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman