1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni ya raia wa Congo baada ya kuongezwa muhula wa Monusco

Mitima Delachance21 Desemba 2021

Umoja wa Mataifa umeongeza muhula mwingine wa mwaka mmoja kwa kikosi cha MONUSCO, huku likikitaka kikosi hicho kufanya kazi hasa zaidi mashariki mwa Congo.

https://p.dw.com/p/44cRn
DRK Nach Überfall auf Konvoi von Luca Attanasio
Picha: Alexis Huguet/Getty Images/AFP

Ni azimio nambari 2612 lililoandaliwa na kupendekezwa na nchi ya Ufaransa ndilo limepitishwa kwa kauli moja na wanachama 15 wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa, likiongeza muda huo wa mwaka mmoja kwa Monusco hadi ifikapo Disemba 20 mwaka 2022, Monusco ikiwa na kiwango cha juu cha wanajeshi elfu kumi na nne mia moja sitini (14.160) na maafisa wa polisi elfu mbili na mmoja (2.001).

Azimio hilo linakitaka kikosi cha MONUSCO kuondoka hadi ifikapo juni mwakani, kutoka jimbo la Tanganyika kusini-mashariki mwa Congo, na kuzidisha juhudi zake huko Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, majimbo matatu ambayo migogoro hadi inaendelea.

Kwa kusisitiza haja ya kuheshimu haki za binaadamu na sheria ya kimataifa ya kibinadamu, baraza la usalama la umoja wa Mataifa linataka kuona ufanisi zaidi wa operesheni za pamoja kati ya majeshi ya Congo FARDC na MONUSCO uwanjani, ikiwa ni pamoja na brigedi yake ya kuingilia kati.

''Kuna juhudi znazofanywa zinazofanywa''

Wanajeshi wa Congo na wale wa umoja wa mataifa kushirikiana katika operesheni za pamoja.
Wanajeshi wa Congo na wale wa umoja wa mataifa kushirikiana katika operesheni za pamoja.Picha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Haya yanajiri wakati huu ambapo katika mkoa wa Kivu Kusini, Monusco imesema kwamba hadi sasa hali ya usalama bado ni ya kutatanisha licha ya juhudi zilizokwishafanyika. Karna Soro ni kiongozi wa ofisi ya Monusco akiwa mjini Bukavu.

"Mwaka huu 2021, sisi, pamoja na mamlaka ya Congo, tuliwaondoa msituni wapiganaji wa Congo 211, na wapiganaji 40 wa kigeni ambao walirejeshwa, wengi wao walirudi Rwanda, wakiwa ni FDLR wa zamani. Kwa bahati mbaya kuna baadhi ya maeneo kama nyanda za juu za Uvira ambako mivutano inaendelea kati ya jamii, kukiwa pia idadi kubwa ya watu waliokimbia makazi yao''

Kuna juhudi zinazofanywa lakini changamoto zinabaki nyingi haswa watu kuishi pamoja kwa amani, likiwa ni suala tete.", alisema 

Lakini raia wa Congo wana maoni tofauti kutokana na uwepo wa Monusco nchini mwao kwa zaidi ya miaka ishirini. Alfred Cibanvunya ni mkaazi wa Bukavu.

Katika azimio lake hilo, baraza la umoja wa mataifa limesema kurizika na ushirikiano ulioongezeka kati ya mamlaka ya Congo, MONUSCO na mataifa jirani, huku likisisitiza umuhimu wa uratibu na upashanaji habari ukijumuisha askari wa ulinzi wa amani wa umoja wa mataifa katika operesheni za kijeshi zinazo fanyika mashariki ya Congo.