1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Ni mchango gani alionao Mandela katika jamii ya sasa?

Sylvia Mwehozi
18 Julai 2018

Nelson Mandela angekuwa anatimiza miaka 100 leo, na wanasiasa wengi wanajaribu kuiga yale aliyoyafanya. Lakini mkuu wa idhaa za Kiafrika za DW Claus Stäcker anauliza ni mchango gani alionao Mandela katika jamii ya sasa? 

https://p.dw.com/p/31dnl
Johannesburg Alexandra Township Mandela Wandbild
Picha: Getty Images/AFP/A. Joe

Rais mstaafu wa Marekani Barack Obama alimsifu Nelson Mandela muda mrefu uliopita kama "dira ya maadili" ya maisha yake ya kisiasa. Obama alilizungumzia hilo kwa mapana na marefu wakati alipohutubia umati wa watu waliojitokeza kwenye uwanja wa Kriketi mjini Johannesburg jana katika ziara yake ya karibuni barani Afrika. Wale walio na shauku zaidi wangeweza kununua kiti wakati wa hafla ya chakula cha jioni ili kumsikia zaidi.

Mandela hakuwa mtu mtakatifu. Lakini licha ya hilo, kila mtu mashuhuri na maarufu aliyekuwa karibu naye alinyenyekea kwake. Mandela alionesha heshima kwa wanamuziki na marais, malkia na walinzi wa gereza. Hadi kipindi anaachiliwa huru kutoka gerezani baada ya kutumikia miaka 27, alikuwa chapa ya dunia, mfano ambao ulimwengu ulikuwa na matarajio makubwa kwake.

Ghafla alisimama katika jukwaa la dunia na kutumia fursa. Tofauti na wengine alikuwa na maono na dira yenye maadili, kama ambavyo alifahamu Obama. 

Hakuwa na kisasi licha ya kifungo kisicho cha haki

Mandela alielezea miaka iliyoonekana kuwa ya milele jela kama "chuo kikuu nyuma ya jela". Nyakati hizo hakuwa na hasira wala mtu mwenye siasa kali. Anasema alijifunza unyenyekevu, na uvumilivu akiwa humo. Baadhi ya wakosoaji kama mwanasiasa machachari Julius Malema, mkuu wa chama cha wapigania uchumi EFF ambaye ni maarufu miongoni mwa raia maskini Afrika Kusini, anasema alijifunza mengi kutoka kwake.

Baada ya miongo miwili si Waafrika Kusini wote ambao wanamudu fursa sawa za mafanikio. Hakuna mahali kokote duniani ambako kuna shida baina ya matajiri na maskini kuzidi Afrika Kusini. Matajiri wazawa na wasomi wa Ulaya wanaishi katika majumba yaliyo na usalama wa hali ya juu "jamii zenye uzio" zikilindwa na polisi ni kama pepo ndogo. Kwa upande mwingine wa muktadha wa kiuchumi, wazawa na wahamiaji wamefungwa katika mapambano ya kikatili ya ubaguzi wa wageni.

Wakati huo huo, sisi wa magharibi hatujaondolewa katika ukweli huo. Jamii zilizojitenga kwa uzio zinazidi kushika kasi barani Ulaya kuliko hapo awali. Matajiri wanajificha katika majumba yao ya kifahari na kisiasa kuwakosoa raia wa kipato cha kati katika vitongoji vyao wakati maeneo yote ya miji ya Ulaya yakibadilika kuwa pointi za kijamii na kisiasa na kuwa na ulimwengu mzuri.

Stäcker Claus Kommentarbild App
Mkuu wa Idhaa za Afrika za DW Claus Stäcker

Pengo baina ya matajiri na maskini linazidi kuwa kubwa. Nchini Ujerumani, ambako nchi inakusanya kodi kubwa, pengo la kielimu baina ya matajiri na maskini linazidi kukua. Watoto kutoka familia ambazo ni maskini wanazaliwa katika hali ambayo haitawapatia fursa ya kung'ara. Kama pengo linazidi kuongezeka katika nchi iliyo na ustawi ya Ujerumani, ni namna gani jamii nyingine ambazo hazina ustawi zitaweza kuendana na hali hiyo?

Ubinafsi wa maandamano

Hii leo  mawazo ya Mandela yameangukia katika kuta za ubinafsi duniani kote. Hadi kufikia karibuni jamii nzima ya urais imevamiwa na nchi kuwapa kinga marais hao. Kutoka Ankara hadi Budabest na Moscow hadi Washington, viongozi walio na ubinafsi wanaendeleza hilo.

Wakati huo huo, mafanikio ya miongo miwili ya mfumo wa uchumi wa masoko ya kijamii na wawakilishi wa kiuchumi yanaonekana kupotea na ushirikiano wa kijamii unafadhaika.

Bila shaka kila jamii lazima ijiulize jinsi gani inavyoweza kuwa na ukarimu. Au ikiwa inaukuchukulia kwa faida. Ikiwa kanuni zake na sheria zinaweza kukubalika na kuhifadhiwa. Ni kiasi gani cha ugeni ambacho inaweza kuvumilia. Na ikiwa haki za waomba hifadhi zinatolewa kwa watu wasio sahihi. Hata hivyo, mjadala wa uhamiaji huku Ulaya umedhoofika kutoka kwenye usambazaji, na kuwa aina ya mjadala wa kujitetea. Kuinua uzio wako na kufunga macho yako! Na kisha uende kwenye darasa lako la yoga ili uwasiliane na mtu wako wa ndani.

Je ulimwengu utaonyesha mshikamano kiasi gani?

Hakuna kuta zitazuia kiu ya kutafuta maisha bora. Lakini si kila mtu anaweza kukimbia, wengi watabaki na kutafuta ufumbuzi mahali waliko. Na bajeti ya waziri wa maendeleo Gerd Müller haitakuwa kubwa kutatua matatizo hayo. Bado swali kubwa la Mandela hii leo ni: Ni mshikamano kiasi gani-tunaweza-kutoa? Mafanikio makubwa ya Nelson Mandela yalikuwa ni kupitisha idiolojia. Kuwa na uwezo wa kusikiliza wengine na kukataa kuona wale walio na msimamo tofauti kama maadui. Hivyo basi kiongozi huyo mwafrika alikuwa mfano wa kuigwa kwa wazungu, wakomunisti, Waislamu na wafanyabiashara.

Bila shaka mtu anaweza kusema hakuna mawazo ya Mandela duniani hivi sasa. Lakini katika siku ya kimataifa ya Mandela swali kubwa la kujiuliza : Ni namna gani Mandela anaishi ndani ya kila mmoja wetu? Tuko tayari kufanya nini? Je tumejiandaa kutoa baadhi ya utajiri wetu na kama ndio ni kiasi gani?

Mwandishi: Claus Stäcker

Tafsiri: Sylvia Mwehozi

Mhariri: Iddi Ssessanga