1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maoni: Msiwanyamazishe wanahabari wakati wa janga la corona

3 Mei 2020

Wakati ulimwengu ukiadhimisha leo Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, wito unatolewa kwa mamlaka kutowakandamiza wahabari ambao wanategemewa katika utoaji wa habari za kusaidia jamii kupambana na janga la corona

https://p.dw.com/p/3bhmx
Deutschland Symbolbild Pressefreiheit
Picha: Imago Images/S. Boness

Tangu kuzuka kwa COVID-19, serikali zimekuwa zikikabiliwa na jukumu kubwa la kuziongoza na kuziendesha jamii kupambana na mojawapo ya migogoro mikubwa kabisa ya nyakati za karibuni, mara nyingi zikilazimika kufanya maamuzi yao kwa kuzingatia maelezo machache ambayo wakati mwingine yanakuwa na utata. Huo ni mtihani mkubwa, ambao una madhara yasiyoonekana  na matokeo yasiyotabirika.

Katika baadhi ya nchi, sintofahamu ya aina hiyo imeongeza tabia ya maafisa kujaribu kudhibiti kila nyanja ya mtiririko wa habari na kuzinyamazisha sauti zisizostahili. Toka mwanzo kabisa mwa janga la COVID-19, kumekuwa na matukio mengi ambapo mamlaka zinaweka hatua, sheria maalum, au amri za kudhibiti haki za wanahabari na vyombo vya habari pamoja na utolewaji huru wa habari.

Hatua hizo ni kuanzia kwa wajibu uliowekwa kwa vyombo vya habari kuchapisha tu habari ambayo imetolewa na mamlaka, kuzifunga tovuti pamoja na kudhibiti upatikanaji wa habari za serikali na kuwaadhibu wanahabari wanaotuhumiwa kwa kusambaza kile kinachoitwa "habari bandia.”

'Suala la kufa na kupona'

Kommentarbild PROVISORISCH OSZE-Beauftragter für die Freiheit der Medien Harlem Desir
Harlem Desir kutoka shirika la OSCE

Wakati wa janga, hasa, upatikanaji wa habari za kweli na za uhakika ni suala la kufa na kupona. Watu wana haki ya kujua kuhusu hatua muhimu za kiafya, takwimu za wazi, na maamuzi ya serikali. Afya ya binaadamu inategemea sio tu kwenye huduma za afya ambazo zinapatikana kwa urahisi, lakini pia upatikanaji wa habari za uhakika kuhusu hali ya vitisho na mbinu ambazo zipo ili mtu kujilinda, familia yake, na jamii yake. Kuzuia utoaji huru wa habari nchini China mwanzoni mwa janga la corona, kwa mfano, hakukuchangia katika kuwalinda watu nchini humo au dunia kwa ujumla. ilikuwa kinyume cha hilo. Tunahitaji habari Zaidi, na sio chache, kutoka kila aina ya vyanzo na kutoka kwa vyombo vya habari vilivyo huru.

Wanahabari wana umuhimu mkubwa katika usambazaji wa habari. Wana jukumu kubwa la kufanya katika kutoa habari muhimu ya afya kwa umma, kubadilisha msamiati au maneno magumu ya kisayansi na kuiweka katika lugha nyepesi  ambayo watu wanaweza kuelewa na kupambana na upotoshaji wa habari.

'Kuficha' habari hakuna faida

Fununu zinaweza tu kukabiliwa vyema kwa kuhakikisha kuna vyanzo vingi vya habari na vilivyo huru. Sidhani kama umma utakuwa na Imani na mamlaka kama zitaonekana kama zinajaribu kuficha habari au kudhibiti vyombo vya habari. Kwa hivyo, badala ya vizuizi Zaidi, tunahitaji uwazi Zaidi. Badala ya kuwanyamazisha wanahabari, mamlaka zinapaswa kuwaacha wafanye kazi yao bila uingiliaji, ziwarhusu kutafuta vyanzo vyote ambavyo vyombo vyenyewe vya habari vitaona vinafaa.

Kisha, serikali zinapaswa kuvipa vyombo vya habari habari za kuaminika. Zinapaswa pia kuvisaidia kifedha vyombo vinavyokabiliwa na matatizo kwa sababu ya janga hili, hasa kwa sababu, katika miaka ya baada ya kumalizika COVID-19, haja ya kazi ya wanahabari haitapungua. Uhuru wa kujieleza na habari, vikiunganishwa na mazingira mapana ya vyombo vya habari, ni wachangiaji muhimu katika ukuaji wa uchumi, na vyombo muhimu katika kuimarisha mahusiano ya kijamii na miundo ya kidemokrasia.

Wakati tukisherehekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 2020, tukumbuke kuwa, katika mgogoro huu wa dharura usio wa kawaida, tunahitaji vyombo huru vya habari kuliko wakati mwingine wowote. Msizinyamazishe sauti huru.

Harlem Desir ni mwakilishi wa uhuru wa vyombo vya habari katika Shirika la Usalama na Ushirikiano Ulaya (OSCE), ambalo ni shirika kubwa kabisa ulimwenguni la masuala ya usalama ya serikali mbalimbali.