1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Manowari ya Marekani yawasili nchini Korea Kusini

Sylvia Mwehozi
22 Juni 2024

Manowari ya Marekani yenye uwezo wa kinyuklia imewasili leo nchini Korea Kusini kwa luteka za kijeshi, zinazonuwia kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini vinavyozidi kuongezeka kutokana na ukaribu wake na Urusi.

https://p.dw.com/p/4hNwe
Manowari Theodore Roosevelt
Manowari ya Marekani ya Theodore Roosevelt Picha: Kham/REUTERS

Manowari ya Marekani yenye uwezo wa kinyuklia imewasili leo nchini Korea Kusini kwa luteka za kijeshi, zinazonuwia kukabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini vinavyozidi kuongezeka kutokana na ukaribu wake na Urusi.

Kuwasili kwa manowari ya Marekani ya Theodore Roosevelt huko mjini Busan, kunakuja siku moja baada ya Korea Kusini kumwita balozi wa Urusi nchini humo kupinga hatua ya kusainiwa mkataba wa ushirikiano baina ya Rais Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Korea Kusini inadai kwamba mkataba huo unatoa kitisho kwa usalama wake na kuonya kwamba itazingatia kuisaidia Ukraine kwa silaha katika mapambano yake dhidi ya uvamizi wa Urusi.

Manowari hiyo inatarajia kushiriki katika luteka za kijeshi zinazotarajiwa kufanyika mwezi huu na kuzihusisha nchi tatu za Marekani, Japan na Korea Kusini.